MSAADA WA MABATI NA MIFUKO YA SARUJI SHULE YA MSINGI KAMBARAGE, NJOMBE.
Tanzania Commercial Bank imetoa msaada wa mabati 60 na mifuko 100 ya saruji katika shule ya Msingi Kambarage iliyopo mkoani Njombe kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 7 na ofisi ya Walimu shuleni hapo. Kaimu Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Uhusiano wa benki Bi. Chichi Banda alikabidhi msaada huo kwa mwalimu mkuu wa shule Bi. Jane Ng'umbi.