Tabasamu
Utangulizi
Katika kutambua umuhimu na changamoto za kujiwekea akiba ambazo watu wengi hukutana nazo, Benki ya Tanzania Commercial Bank
Madhumuni
Kuwezesha akina mama na .akina dada kujikwamua kiuchumi kwa kufungua akaunti ya TABASAMU iii kujiwekea akiba na hatimaye kuboresha maisha yao ya kila siku kwa kuongeza mitaji ya biashara zao/au kuanzisha shughuli mbali mbali za kiuchumi.
Walengwa wa akaunti hii
Akaunti hii ni mahsusi kwa akina mama au akina dada wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi za aina yoyote (biashara), waajiriwa, walio katika kikundi au mtu mmoja mmoja
Mahitaji ya Kufungua Akaunti ya TABASAMU
1) Kwa Mtu mmoja mmoja
(a) NAKALA ya kitambulisho cha Utaifa, au Kadi ya mpiga Kura au Leseni ya Udereva au Hati ya Kusafiria
(b) Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/makazi au ankara ya malipo ya Umeme au malipo ya maji kuthibitisha eneo unalotoka
(C) Picha mbili za kipimo cha hati ya kusafiria Cnyuma yenye rangi ya buluu),
(d) Kiwango cha kufungulia akaunti hiini 10,000/=
(e) Gharama za uendeshaji ni 4,000/= tu.
2) Kwa Kikundi cha TABASAMU
a) Kikundi Rasmi-Kilichosajiliwa
i. Barua ya utambulisho toka kwenye kikundi
ii. Orodha ya wanachama wa kikundi na·sahihi zao
iii. Muhutasari wa kikundi kuonesha uteuzi wa waendesha akaunti
iv. Picha za waendesha akaunti
v. Katiba ya kikundi
vi. Kiwango cha kufungulia akaunti hii ni 50,000/=
vii. Gharama za uendeshaji ni 30,000/= tu.
b) Kikundi Kisicho rasmi-kisichosajiliwa
i. Muhutasari wa kikundi wenye majina ya wanakikundi na sahihi zao
ii. Barua toka kwa kiongozi wa kikundi kuelekezwa Tanzania Commercial Bank ikionesha dhamira ya kutaka kufungua akaunti, majina ya waendesha akaunti kama ilivyokubalika kwenye kikao
iii. Picha za waendesha akaunti ambayo imepigwa hivi karibuni kwa madhumuni ya·kufungua akaunti
iv. Katiba ya kikundi (kama ipo)
Faida za kuwa na akaunti ya TABASAMU
Akaunti ya TABASAMU inampa fursa mwenye akaunti kuchukuwa mkopo hadi asilimia hamsini (50%) ya akiba yake mara anapohitaji kufanya hivyo
i. lnatoa faida nono kwa mwaka
ii. Inampa mwenye akaunti kinga ya BIMA ya Maisha
iii. Akaunti ya TABASAMU inatumika kama dhamana endapo mwenye akaunti anahitaji mkopo