MSAADA WA MABATI SHULE YA MSINGI KATAVI

Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Tanzania Commercial Bank tumetoa msaada wa mabati bando kumi na tano yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Milioni Tano na laki Nne kwa shule ya Msingi Katavi iliyopo Mkoa wa Katavi Manispaa ya Mpanda.

Dhumuni la Msaada huo ni kuisaidia shule kupaua madarasa mawili ili Wanafunzi wasome katika mazingira bora.

Aliyepokea msaada huo kwa niaba ya shule ni Afisa Elimu Mkoa Dr. Elipidius Baganda (katikati) ambaye alikabiziwa mabati hayo na Bi. Grace Majige (kulia), Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki. Wengine kwenye picha ni Diwani wa kata ya Makanyagio na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Haidari Sumri (wa kwanza kushoto), Meneja wa Tawi la Mpanda Bw. Julius Mlanga na Mwalimu Mkuu Bw. Wailes Kibona.

Location

Head Office 10th LAPF Towers,
Bagamoyo Road, Opp Makumbusho Village,
Kijitonyama,
P.O BOX 9300, Dar es salaam

Call Center

+255 765 767 683
+255 788 767 683
+255 658 767 683
+255 773 767 683

Email Us

info@tcbbank.co.tz,
callcentre@tcbbank.co.tz,