MSAADA WA MAJENGO YA VYOO SHULE YA MSINGI IFWAGI
Tanzania Commercial Bank imekabidhi majengo ya vyoo yenye matundu 20 (10 Wanafunzi wakike, 8 wa kiume na 2 Walimu) katika Shule ya Msingi Ifwagi iliyopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Mradi huo ulikabidhiwa rasmi kwa uongozi wa Shule na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka benki ya Biashara Tanzania Bi. Diana Myonga katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.