MSAADA WA MABATI KWA MAGEREZA MASASI
Tanzania Commercial Bank imekabidhi mabati Mia mbili yenye thamani ya Shilingi milioni saba na laki nane kwa Magereza Wilaya ya Masasi ambayo yatatumika kuezekea Hospitali inayojengwa na Magereza hiyo. Kwenye picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Ndg. Sabasaba Moshingi akikabidhi mabati hayo kwa Mh. Geofrey Mwambe, Waziri wa Uwekezaji na Mbunge wa Masasi aliyepokea kwa niaba ya Magereza hiyo.