MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI MARIWANDA A
Tanzania Commercial Bank imetoa msaada wa madawati katika Shule ya Msingi Mariwanda A iliyopo Wilayani Bunda mkoani Mara. Msaada huo utaenda kuwasaidia Wanafunzi 150 katika shule hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Joshua Nassari alipokea madawati hayo kwa niaba ya Shule kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki Musoma Bw. Hagai Gilbert.