MSAADA WA MAHITAJI MAALUMU KWA WATOTO YATIMA NA WENYE ULEMAVU SHULE YA MSINGI PONGWE TANGA
Katika kusherehekea siku ya Mtoto wa Africa, Tanzania Commercial Bank imetoa msaada wa mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Pongwe mkoani Tanga. Meneja wa Tawi la Tanga Bw. Patrick Swenya pamoja na Wafanyakazi wengine wa benki walihudhuria tukio hilo muhimu linalosherehekewa dunia nzima.