MSAADA WA SARUJI HOSPITALI YA BUGANDO
Tanzania Commercial Bank imekabidhi msaada wa tani 25 za mifuko ya saruji katika Hospitali ya rufaa ya Bugando mkoani Mwanza kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa wodi ya saratani hospitalini hapo. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Ndg. Sabasaba Moshingi.