MSAADA WA VITI NA MEZA SHULE YA SEKONDARI UBAGWE, MKOANI SHINYANGA.
Benki imetoa msaada wa viti 92 na meza 92 kwa shule ya Sekondari Ubagwe iliyopo katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Mkurugenzi wa mikopo wa Tanzania Commercial Bank, Bw. Henry Bwogi alikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha aliyepokea kwa niaba ya shule hiyo.