MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI SHULE YA MWEMBENI MANYONI
Tanzania Commercial Bank imekabidhi vifaa vya ujenzi Shule ya Mwembeni Manyoni kwa ajili ya kumalizia jengo la shule. Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Bw. Iddi John, Meneja wa tawi la Benki la Manyoni ambaye amemkabidhi Bw. Simon Mwarabu ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Mwembeni.