MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI KOMBOA, WILAYA YA MBINGA MKOANI RUVUMA
Tanzania Commercial Bank imetoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya Sh. milioni 4.3 kwa shule ya Msingi Komboa iliyopo kijiji cha Ruanda Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma. Madawati hayo yalikabidhiwa na Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Tanzania Commercial Bank kwa Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini.