MSAADA WA MAHITAJI MAALUM KAMBI YA WANAFUNZI KIDATO CHA 6 NA 4 MKOA WA SIMIYU.
Benki imetoa msaada wa mahitaji maalum kwa kambi ya Wanafunzi wa kidato cha 6 na 4 katika Mkoa wa Simiyu. Mahitaji hayo yenye thamani ya Shilingi Milioni 4 na laki 5 yaliyopokelewa na Kaimu RAS wa Simiyu Bw. Ekwabi Majungu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB Bw. Henry Bwogi. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika shule ya Sekondari Bariadi mkoani Simiyu.