MSAADA WA CEMENT PEMBA
Tanzania Commercial Bank imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya Mavungwa Pemba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 2.6 kwa lengo la Wawezeshe kujenga shule hiyo. Vifaa hivyo vilijumuisha Matofali na Cement vilikabidhiwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki Bi. Grace Majige na Meneja wa tawi la Pemba Ndg. Shomary Rimisho.