MSAADA WA CEMENT MTO WA MBU
Tanzania Commercial Bank imekabidhi mifuko 100 ya Cement kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei Mto wa Mbu Mkoani Arusha. Lengo la msaada huo ni kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo lililo karibu na tawi letu la Mto wa Mbu.
Kwenye picha ni Bi. Grace Majige, Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki na Ndg. Ignas Mkawe, Meneja wa tawi la Mto wa Mbu wakikabidhi kwa Paroko wa kanisa hilo Father Peter Kwayu.