UJENZI NA UKARABATI SHULE YA MSINGI NANDAGALA, RUANGWA.
Tanzania Commercial Bank imemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) vyumba 11 vya madarasa, ofisi 2 za waalimu, samani na chumba maalum cha wasichana wa kike katika Shule ya Msingi Nandagala iliyopo katika kijiji cha Nandagala B Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Mradi uliogharimu Milioni 164.9 inayojumuisha ujenzi pamoja na ukarabati.