MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI UMOJA - TUNDURU
Benki ya Biashara Tanzania imetoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya fedha za kitanzania Tshs milioni tano. Hafla hiyo ilisimamiwa na Meneja wa Tawi la Tunduru Emajacquline Mtambo na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Ndg. Julius S. Mtatiro kwa ajili ya kuwasaidia Shule ya Msingi Umoja kuepukana na changamoto za kukaa chini na ikiwa ni moja ya mpango wa Benki kuunga mkono sekta ya Elimu.