MSAADA WA VITI 25 PAMOJA NA MEZA 25 SHULE YA SEKONDARI KIPAGAMO
Benki ya Biashara Tanzania kupitia Tawi la Makambako ilifanikiwa kukabidhi msaada wa viti ishirini na tano (25) na meza ishirini na tano (25) katika shule ya sekondari kipagamo iliyopo Makambako. Mgeni rasmi katika hafla hii fupi alikua mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Makambako Mh. Hanana Mfikwana kuwakilishwa na Mh. Diwani John .E. Ngimbudzi.