MSAADA WA MABATI 288 - KITUO CHA AFYA ISANGU MBOZI
Benki ya Biashara Tanzania ( TCB Bank Plc) imekabidhi mabati 288 katika kituo cha Afya kata ya Isangu, Mbozi.
Vifaa vilikabidhiwa katika kijiji hicho na Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Diwani wa kata ya Hasana Bw. Mirick Nzowa na Meneja wa Benki Tawi la Mwanjelwa Bw. Simon Mlelwa na Meneja Tawi la Mbeya Bw. Eric Mjuni.