MCHANGO WA VIFAA VYA UJENZI - SHULE YA MSINGI MLABANI IFAKARA
Benki ya TCB kuipitia Tawi la Ifakara, ilikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchangia uendelezi wa ukarabati wa madara chakavu yaliyopo kwenye shule hiyo.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Shule Bw. Abasi Gora kwenye picha ni Meneja wa Tawi la Ifakara Bi. Frida Sanga, Uongozi wa Shule na Kamati ya Wazazi.