UKARABATI WA MADARASA MATATU NA OFISI MBILI ZA WALIMU
Benki yetu ilipiga hatua katika kukamilisha mradi wa ukarabati wa madarasa matatu na ofisi mbili za walimu katika shule ya msingi Muyama, iliyopo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Ikiwa ni moja ya sera ya Benki kutoa kwa jamii (CSR), ilitembelea shule hiyo ambayo ilikua na madarasa chakavu ambayo sio salama kwa wanafunzi, hivyo ikaona ni vyema kutoa msaada wa kukarabati madarasa hayo.
Sambamba na hiyo benki ilichangia madawati Ishirini na Tano ili kupunguza msongo wa wanafunzi kwenye dawati moja, na kutoa msaada wa Printer moja kwa ajili ya walimu.