UJENZI WA MAJENGO YA VYOO SHULE YA MSINGI KIKELELWA - ROMBO
Kwa kutambua jitihada za Serikali, Benki ilipata fursa ya kutatua changamoto zinazoibakili wilaya ya Rombo kwenye Sekta ya Elimu kwa uchache wa matundu ya vyoo ambayo awali yalikua kwenye mazingira hafifu.
Tumejenga vyoo vya wasichana na wavulana shule ya Msingi Kikelelwa baada ya kuona changamoto ya hali mbovu ya vyoo vilivyokua hapo awali. Tulifanya hafla fupi ya kukabidhi majengo hayo kwa Halmashauri ya Rombo.