SABASABA TRADEFAIR EXHIBITIONS 2021
Tanzania Commercial Bank ilishiriki maonesho ya biashara ya Sabasaba yaliyofanyika mwaka huu kwenye viwanja vya Sabasaba Kurasini. Benki ilipata fursa ya kutoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha, kubadili fedha za kigeni, kupata huduma za kutuma na kupokea kupitia Western Union, huduma za bima, huduma za mikopo, n.k.