TCB BANK NA LETSHEGO BANK KUINGIA MKATABA
Tanzania Commercial Bank na Letshego Bank Tanzania zimekubaliana kuanza kufanya kazi kwa karibu ili ushirikiano wao wa kibiashara uwe ni wa manufaa makubwa na tija katika kusambaza huduma za kibenki kwa wateja nchini.
Katika kulitimiza hilo, jana benki hizo ziliingia makubaliano yanayowawezesha wateja wa Letshego kuweka pesa kwenye akaunti zao kupitia matawi ya TCB.