TAWI LA USARIVER
Tanzania Commercial Bank imesherekea uzinduzi wa Tawi lake la Usariver Tarehe 11 Machi, 2022 katika wilaya ya Usariver mkoani Arusha. Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alizinduwa tawi hilo kwa kukata utepe na kufungua jiwe la Msingi. Tawi la USA River lilianzishwa mwaka 2007 kwenye ofisi za posta, Usariver ikiwa ni benki ya kwanza kufika na kutoa huduma za kifedha katika wilaya ya Arumeru.